TANGAZA NASI HAPA

Wednesday, 1 March 2017

NUSU FAINALI YA PILI COPPA ITALIA; ‘Derby della Capitale’ kulisimamisha jiji la Roma, ni Lazio vs Roma Leo




AS Roma  imeshinda  michezo  mitano  kati  ya  sita  ya  mwisho  katika ‘Derby della Capitale’ dhidi  ya  mahasimu  wao  wa  jiji ‘Takatifu’ la  Roma, SS Lazio. Michezo  sita  ya  mwisho  kati  ya  timu  hizo  ilikuwa  katika  Serie  A na  Lazio  wamefanikiwa  kuambulia  sare  moja  tu,  Januari  11, 2015  walipofungana  2-2.

Timu  hizo  zinakutana  tena  usiku  wa  Jumatano  hii  katika mchezo  wa  nusu  fainali  ya  kwanza michuano  ya  Coppa  Italia  huku  Lazio  wakiwa  wenyeji katika  uwanja  wa  Estadio  Olimpico. Lazio  imepoteza  michezo  yote  mitatu  ya  mwisho  baina  yao  ambayo  walikuwa  wenyeji huku  kipigo  cha  mwisho  wakipata Desemba 4, 2016 kwa  kulazwa  2-0.
 Simone Inzaghi (kaka  wa  Phillipo  Inzaghi) aliiongoza  timu  yake  kuwatoa  Inter  Milan  katika  hatua  ya  robo  fainali mwezi  uliopita anamtegemea  zaidi  mshambulizi, Ciro Immobile, kiungo  Muargentina Lucas Bilglia huku  kikosi  chake  kikiwa  kimeshinda michezo minne  na  kupata  sare  moja  katika  game  tano   za  mwisho  katika  michuano  yote. 
 Luciano Spalletti ambaye  timu  yake  iliitoa  Cecena  katika  robo  fainali anaweza  kumuanzisha  mkongwe  Francisco Totti na  Stephan El Shaarawy ambao  wamekuwa  wakitumika  zaidi  katika  michuano  hiyo  lakini  pia   anaweza  kubadili  uamuzi  na  kupanga  safu  yake  hatari  ya  mashambulizi ambayo  imefunga  magoli  11  katika  michezo  minne iliyopita.

Edin Dzeko anaweza  kusimama  kama  mshambulizi  pekee,  huku  katikati  wakipangwa  viungo  watano Mohamed  Salah, nahodha  Daniele De  Rossi, Kevin Strootman, Bruno  Perez  na  Radja  Nainggolan ambao  walianza  katika  mchezo  wa  ushindi  wa  3-1  ugenini  dhidi  ya  Inter  Milan  katika  ligi  kuu Jumapili  iliyopita.

 
Mechi  ya  Lazio  dhidi  ya  Roma  ni  kati  ya  michezo  mitano  bora  ya  ‘wapinzani wa  jadi’  duniani huku  mipambano  yao  ikizusha  vurugu  za  mara  kwa  mara  ndani  na  nje  ya  uwanja.

No comments:

Post a Comment