BARCELONA imekuwa timu ya kwanza barani ulaya kupindua
matokeo ya 4-0 na kufuzu kwa hatua inayofuata ya michuano ya ligi ya mabingwa.
Magoli matatu ndani ya dakika tatu za mwisho kutoka kwa Neymar Jr dakika za 88’ na 90’
alilofunga kwanjia ya penalty na lile la mwisho kutoka kwa Sergi Roberto yameipeleka Barca robo fainali baada ya
kushinda 6-1 usiku wa Jumatano na kufuzu kwa matokeo ya jumla 6-5 dhidi ya PSG.
Neymar alitajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Luis Suarez alifunga goli la kuongoza dakika ya 3’ tu ya mchezo,mlinzi Layvin
Kurzawa akajifunga dakika ya 40’ na kufanya mchezo kwenda mapumziko Barcelona
wakiongoza 2-0. Kocha Luis Enrique
alibadilisha mfumo wa kiuchezaji ambao ulimfanya Lionel Messi kucheza
eneo la kiungo.
Enrique aliwapanga
walinzi watatu nyuma,Samuel Umtiti, Javier Madcherano na Gerlad Pique. Katika kiungo
akawapanga Messi,nahodha Andres Iniesta, Sergio Busquets na Ivan Rakitic huku
washambuliaji wakiwapangwa Rafihna Alcantara, Suarez na Neymar.
Messi alifunga goli la tatu kwa mkwaju wa penalty dakika ya
50’ . mshambulizi Edson Cavanni alifunga alimalizia pasi ya Kurzawa dakika ya
62 na kuwafungia Waparis hao goli muhimu la ugenini na bao hilo lilimaanisha
Barca inapaswa kushinda kuanzia 6-1.
Dakika zikiwa zimeyoyoma Neymar akafunga mara mbili kasha Roberto
akamalizia goli muhimu zaidi dakika ya mwisho akimalizia pasi ya Neymar na
kuifanya Barca kushinda 6-1 na kuwatupa
nje mabingwa hao wa Ligue 1.
No comments:
Post a Comment