TANGAZA NASI HAPA
Friday, 3 March 2017
‘ Hali mbaya uchumi klabuni imesababisha kusitishwa kwa ajira yangu Yanga SC’-Hans vander Pluijm
UONGOZI wa klabu bingwa Tanzania bara, Yanga SC umesitisha ajira ya Mholland, Hans van der Pluijm ambaye alikuwa Mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo. Hans ambaye aliifundisha Yanga kwa miaka miwili na kuipa mataji mawili ya VPL, moja la FA Cup amethibisha kupewa barau ya kuachishwa kazi na sasa yuko huru kufanya kazi na klabu yoyote atakayokubaliana nayo.
“Nimepewa barua asubuhi hii na Yanga juu ya mkataba wangu kuwa umesitishwa, kikubwa walichokisema ni kuwa klabu kwa sasa inakabiliwa na ukata hivyo hawana uwezo wa kuendelea kunilipa.Kwa sasa nipo huru kujiunga na klabu yoyote itakayoonyesha nia na mimi basi nitafanya nao kazi.” anasema Mdach huyo mwenye miaka 68.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment