WAKICHEZA pungufu
mchezaji mmoja kwa
zaidi ya dakika
45, mabingwa watetezi wa
ligi kuu Tanzania
Bara, Yanga SC wamefanikiwa
kushinda 2-0 dhidi ya
Ruvu Shooting katika mchezo
uliopigwa uwanja wa Taifa Dar
es Salaam jioni hii huku mlinzi
wa kati raia
wa Togo, Vicent Bossou
akicheza kwa kiwango
kizuri.
Mshambulizi raia wa
Zambia Obrey Chirwa
alioneshwa kadi ya
njano dakika ya 44 kwa kosa la kufunga goli kwa mkono na kumsukuma golikipa
wa Shooting, Bidii Hussein na
dakika moja baadae
akapewa ya pili ya njano
iliyoambatana na kadi nyekundu na
mwamuzi, Ahmada Simba kwa
kosa la kuutupa
mpira chini kwa hasira
na kuwaacha pungufu wenzake.
Kiungo mshambulizi, Saimon
Msuva alifunga goli
lake la 12
msimu huu kwa
njia ya mkwaju
wa penalty dakika
ya 32. Goli hilo
lilidumu hadi kipindi cha
kwanza kinamalizika. Mtokea benchi, Emmanuel Martin
akaongeza goli la
pili dakika ya
90’. Martin aliingia dakika 12
kabla ya kumalizika
kwa mchezo akichukua
nafasi ya Deus Kaseke.
Kwa matokeo hayo Yanga
imefikisha pointi 52 baada
ya kucheza michezo
23 (pointi mbili nyuma
ya vinara Simba SC) Mwishoni
mwa wiki hii
kikosi cha kocha
George Lwandamina kitaivaa
Mtibwa Sugar katika
uwanja wa Jamhuri, Morogoro wakati
Simba watacheza na
Mbeya City FC
katika uwanja wa Taifa.
No comments:
Post a Comment