Na Baraka Mbolembole
HATA kabla ya mabadiliko ya kutoka na
kuingia Deus Kaseke dakika za mwisho tayari ‘nilishang’amua’ uwezo mdogo wa
kocha George Lwandamina.
Mkufunzi huyo mkuu wa Yanga SC raia wa
Zamabia sasa atahitaji kufanya
‘ushawishi’ mkubwa kwa mashabiki wa timu hiyo ili kumuamini kuwa ni ‘kocha
sahihi’ wa kuisogeza mbele timu bora iliyoachwa na mtangulizi wake
Mholland,Hans van der Pluijm.
Kila mtazamaji wa mchezo wa Jumamosi hiii
kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Zanaco FC kutoka Zambia alifurahishwa na uwezo
wa juu ulioneshwa na kiungo mchezesha
timu wa Zanaco, Zimbseleni Moyo ambaye alitawala kiungo katika mchezo huo wa
kwanza hatua ya mwisho ya mtoano kuwania
kufuzu kwa makundi.
Kila ‘Mzalendo’ alitaraji matokeo bora kwa
wawakilishi hao wa Tanzania Bara,lakini wengi waliishia kulaumu kiwango cha
timu ndani ya uwanja na timu ya ushindi. Siku mbili kabla ya mechi niliandika
kwamba kocha wa Yanga, Lwandamina na
wasaidizi wanapaswa kuundaa ‘timu mpya ya mpito’ kutokana na wachezaji wengi
muhimu kuwa na majeraha.
Licha ya ‘kulazimishwa kucheza’ huku wakiwa
na maumivu Wazimbabwe, Donald Ngoma na
Thaban Kamusoko kikosi cha Yanga kilionekana kitakabaliwa na ‘mchezo mgumu’
katika uwanja wa nyumbani mbele ya mabingwa hao wa Zambia, huku habari za
wachezaji kupoteza morali kutokana na ukosefu wa mishahara zikiongeza wasiwasi
kama kweli timu iko tayari kwa mchezo huo muhimu.
Presha bila shaka ilikuwa kubwa kwa
Lwandamina,huku kuwakosa wachezaji wake Amis Tambwe,Haruna Niyonzima
kukimaanisha timu ‘itakosa makali’ katika ushambuliaji na ufungaji.
Bila Ngoma aliye katika makali, Yanga
ilianza mchezo ikiwa na mshambulizi mmoja, viungo wawawili wa pembeni ( Saimon
Msuva na Obrey Chirwa,) na viungo watatu katikati ya uwanja ( Kelvin Yondan,
Justine Zulu na Thaban.) Hassan Kessy na Mwinyi Hajji katika beki za
pembeni,nahodha Kelvin Yondan na Vicent Bossou katika ulinzi wa kati.
Katika benchi walikuwepo golikipa Ally
Mustapha, walinzi watatu Oscar Joshua, Juma Abdul, na Vicent Andrew, pia
walikuwepo viungo watatu wa mashambulizi, Deus Kaseke, Juma Mahadhi na Emmanuel
Martin ambao wote walipata nafasi ya kucheza kipindi cha pili.
Katika muda wote wa dakika 60’ alizokuwa
uwanjani,Ngoma alikuwa ‘mtu wa mashabiki’ wa Yanga na ‘hakubanduka midomoni
mwao’ hata pale alipotolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mahadhi. Ngoma
alionekana ‘kupwaya’ katika mfumo ambao
ulimfanya acheze kama mshambulizi pekee, huku Kamusoko akicheza nyuma yake.
Alipokuwa akigusa mpira alionekana hayupo
‘fiti’na nafikiri hata kocha Lwandamina alikosea kumpanga mshambulizi huyo
pekee. Kwa kutambua majeraha aliyonayo,Lwandamina alipaswa kumpanga Ngoma
sambamba na Chirwa katika mfumo wa 4-4-2 ili kumsaidia mchezaji huyo
‘aliyejitolea kuccheza japokuwa hayupo tayari kimwili.’
Ndiyo,Ngoma alionresha kiwango cha
kufadhaisha sana lakini uwepo wake uwanjani uliisaidia Yanga kuwa salama kwa
sababu wachezaji wa Zanaco wanafahamu kuhusu makali yake katika ufungaji. Hivyo
hawakusogea kwenda mbele.
Upande wangu nitaendelea kumlaumu kocha
Lwandamina kwa sababu hakujiandaa kukabiliana na majeraha yanayoisumbua timu yake,na ni yeye ndiye
sababu ya kiwango kibovu cha timu. Wachezaji wengi wamekuwa wakilalamikia
nafasi wanazochezeshwa na kocha huyo,jambo ambalo limefanya washindwe kutoa
matokeo mazuri kama ilivyokuwa wakati wa Hans van der Pluijm.
Mfumo wa kumpanga Ngoma pekee wakati akiwa
na majeraha uliimaliza timu ndiyo maana mpira haukuwa ukikaa mbele walau kwa
dakika moja tu. Ndiyo wachezaji wanaweza kufanya vyema katika mfumo wowote,
lakini si rahisi ikiwa hawapo ‘fit’ kimwili na kiakili. Ngoma amecheza mara
kadhaa kama mshambulizi ‘huru’ wakati wa Hans na alifanya vizuri kwa sababu
alicheza akiwa bila maumivu.
Bahati mbaya kwa Lwandamina ni kwamba Ngoma
na Kamusoko walicheza pasipo kujiamini na wakati mechi ikiendelea wakaonekana
hadi na wapinzani wao kwamba hawako ‘fit’ Lwandamina alianza kupunguza makali
ya timu kutokana na mfumo wake na kutowaamini vijana wenye vipaji kama Hassan
Mhilu ambaye angeweza kufanya vizuri zaidi ya Kelvin Yondan ambaye alichezeshwa
namba sita.
Baada ya kipigo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC
katika michuano ya Mapinduzi Cupmapema mwezi Januari nilianza kujenga hofu
kuhusu mbinu za Lwandamina,mechi mbili alizoisimamia Yanga vs Simba ( Mapinduzi
Cup na ligi kuu,) na baadaye suluhu-tasa dhidi ya Mtibwa sikuwana shaka tena
zaidi ya kuamini chini ya Mzambia huyu Yanga itapata wakati mgumu.
Sasa timu ambayo ilikuwa katika kiwango cha
juu kiuchezaji,hamasa,uwajibikaji imebadilika huku wachezaji wakiendelea
kushuka viwango kila leo. Kama wachezaji wanashuka viwango hii inamaanisha kuwa
uwezo wa kocha nimdogo.
Upande wangu ni mmoja kati ya
wanaohitajimatokeo bora,kocha kama huna uwezo wa kupanga kikosi na kufanya
mabadiliko basi ‘hukidhi’mahitaji ya timu. Lwandamina alipaswa kumuanzisha Deus
Kaseke au Mhilu katika wing mojawapo sambamba na Saimon Msuva huku Ngoma na
Chirwa wakicheza kama washambuliaji ‘wanaotegemeana.’
Unapokutana na timu iliyo bora katika
kiungo,kama ilivyokuwa kwa Zanaco alafu unamtoa mchezaji kama Kamusoko ambaye
alikuwa bora kuliko wote upande wako na kumuingiza Mahadhi ambaye hana uwezo
mkubwa wa kukaa katikati ya uwanja, ni dalili za kuwafanya watu waendelee
kuhoji kuhusu uwezo wa Lwandamina.
Inakuwaje aliingiza timu yake katika mfumo
wa kuzuia katika uwanja wa nyumbani? Lwandamina hakupaswa kujaribu mfumo katika
mechi muhimu,na alipaswa kumuweka benchi Kelvin au ili kutoa nafasi kwa
wachezaji asilia wa nafasi ya kiungo kuchukua mipira nyuma na kuipeleka mbele
jambo ambalo Kelvin alishindwa na matokeo yake mipira ikawa inapigwa kutoka
nyuma kwenda mbele bila mpangilio wa mashambulizi.
Kiwango cha chini walichoonesha Yanga
katika mchezo wa kwanza kimezua wasiwasi kama kwelitimu hiyo itaweza kusonga
mbele ikicheza ugenini. Walizuia vibaya,walipanga mashambulizi vibaya,na hawakuwana
ubora katika mashambulizi.
No comments:
Post a Comment