BAADA ya kupoteza uongozi wa 4-0 walioupata katika mchezo wa
kwanza jijini Paris kocha wa Paris St.German, Unal Emery amesema kipigo cha 6-1
walichokumbana nacho Nou Camp kutoka kwa FC Barcelona kimemuumiza kila mmoja
katika klabu yake.
Paris imeondolewa kwa jumla ya magoli 6-5 na kushindwa kwa
mara ya tatu kuwaondoa Barcelona katika michuano ya mabingwa ulaya usiku wa
Jumatano hii.
Magoli matatu ndani ya dakika tatu za mwisho yaliyofungwa na
Neymar Jr aliyefunga mawili dakika za 88’ na 90’na lile la Sergio Roberto
dakika ya mwisho ya mchezo yamewaumiza mmno wapenzi wa timu hiyo ya Ufaransa.
“Tumepoteza nafasi nzuri ya kusonga mbele. Tulitaka kukua kulingana na mchezo, kipindi cha kwanza hatukucheza kwa kiwango tulichotaka. Tulitaka kucheza kama mchezo wa kwanza, tulitaka kucheza mtindo wa counter-attack. Baada ya goli la tatu timu ilikuwa vizuri, tulihitaji kupata matokeo mazuri kwa kufunga goli la pili.”
“Ndani ya dakika tano, tulipoteza kila kitu. Hatukuwa na uwezo wa kujilinda. Ni experience mbaya kwetu, lakini ni somo. Najifunza kupitia kushindwa, ni wazi tumepoteza fursa nzuri.”
No comments:
Post a Comment