TANGAZA NASI HAPA

Wednesday, 1 March 2017

HAMASA: Manchester United kuwalipia mashabiki safari ya Urusi


KUELEKEA mchezo wao wa  hatua  ya 16 katika  michuano ya Europa League dhidi ya  Warusi, Rostov klabu ya Manchester  United ili kuhakikisha kuwa wanaendelea kupata sapoti ya mashabiki klabu hiyo  imepanga kulipa gharama zote ambazo mashabiki wataingia kulipia Visa za Urusi kwa mashabiki watakaosafiri kwenye mchezo dhidi ya FC Rostov utakaofanyika March 9.

Manchester United watasafiri mpaka Rostov, klabu ambayo ipo umbali wa takaribani maili 2,000 Mashariki mwa Ukraine, kwa ajili ya mchezo wa raundi ya 16 bora na mashabiki takribani 500 wanatarajiwa kusafiri kwa ajili ya mchezo huu.
 Klabu hiyo imepanga kulipa kiasi cha paundi 118.20 (£118.20) ambayo ni gharama ya kupatikana kwa Visa ya Urusi ikiwa ni ishara ya kuwathamini mashabiki ikiwa ni kutambua muda mchache wa mashabiki kujiandaa kwani ni wiki tatu tu zilizopo kati ya droo na mchezo wenyewe.

No comments:

Post a Comment