Katika mchezo wa
kwanza wa nusu fainali baina ya mahasimu wa jiji la
Rome, SS Lazio imefanikiwa kuibuka na ushindi
wa magoli 2-0 katika ‘Derby della Capitale’
dhidi ya AS Roma katika uwanja
wa Estadio Olimpico, Rome.
Sergej Milinkovic-Savic
alifunga goli la
kwanza dakika ya 29’, dakika
12 kabla
ya kumalizika kwa
mchezo mshambulizi wa
Italia, Ciro Immobile
akafunga goli la
pili katika mchezo
huo wa Derby. Timu hizo
zitarudiana wiki mbili zijazo .
No comments:
Post a Comment