Kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa Afrika siku ya kesho
katu ya wenyeji Yanga SC vs Zanaco FC ya Zambia kocha msaidizi wa mabingwa hao
wa Tanzania Bara,Juma Mwambusi amesema kuna asilimia 50 tu za kuwatumia
washambuliaji wao wa kigeni Mzimbabwe, Donald Ngoma na Mrundi, Amis Tambwe.
Washambuliaji hao wawili wamekuwa wakisumbuliwa na maumivu.
Ngoma amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti sawa na Tambwe, lakini kuna
uhakika wa kiungoMzimbabwe Thaban Kamusoko kucheza mchezo huo muhimu kwa
wawakilishi hao wa Bara.
“ Tunakwenda kucheza mechi ngumu ya hatua ya mtoano,
tunacheza nyumbani. Tunashukuru maandalizi yanakwenda vizuri hadi sasa pamoja
na uwepowa majeruhi na wachezaji
waliokuwa na majeraha. Kikubwa kuna wachezaji ambao kila siku walikuwa
wakifanya mazoezi vizuri, wako tayari kwa mchezo.”
“ Kwa wale wachezaji waliokuwa na majeraha kwa muda mrefu
tunaendelea kutazama maendeleo yao,bado kuna siku moja ya kuendelea
kujilidhisha kuhusu utayari wao wa kushirikimchezowa Jumamosi, vinginevyo Yanga
ina kikosi kipana,kwa hiyo wachezaji wengine waliopo wanaweza kutuwakilisha
vizuri katika mchezo wetu.”
“ Tumeshacheza michezo mingi bila ya wachezaji waliokuwa na
majeraha na tukapata matokeo, hivyo
ieleweke kabisa wachezaji waliosajiliwa Yanga wote wanaweza kuitumikia timu vizuri. Tumeona
Ngoma amerudi lakini hatujajua kama anaweza kucheza, Tambwe alikuwa najeraha la
mguu lakini ameanza mazoezi kwa hiyo naweza kusema wachezaji hawa wako na
asilimia 50 kwa 50 kucheza mchezo ujao lakini Kamusoko atakuwa tayari kucheza
kwa sababu maumivu yake yamepungua kwa kiasi kikubwa.”
No comments:
Post a Comment