WAKATI Simba SC ikitaraji kucheza na Mbeya City FC siku ya
kesho Jumamosi katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, msemaji wa timu hiyo
Hajji Manara na meneja wa timu Musa Hassan Mgosi jioni hii ( leo Ijumaa) wameonekana
ARC Hotel iliyopo Morogoro pamoja na baadhi ya wachezaji wa Mtibwa Sugar.
Mtibwa itacheza na Yanga SC siku ya Jumapili katika
muendelezo wa michezo ya ligi kuu na kuna uwezekano viongozi hao wa Simba ‘wamekwenda’
kuweka 'hasama' ili timu hiyo iisimamishe Yanga ambao wanakimbizana na Simba
katika mbio za ubingwa wa ligi kuu msimu huu.
Simba wanaongoza ligi hiyo kwa tofauti ya pointi mbili mbele
ya Yanga huku kila timu ikiwa imeshacheza jumla ya michezo 23.
No comments:
Post a Comment