MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania
Bara, Yanga SC imeshindwa kurejea kileleni mwa msimamo baada ya kulazimishwa
suluhu-tasa dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri,
Morogoro jioni hii.
Kiungo-mshmbulizi, Saimon Msuva alipaisha mkwaju
wa penalti dakika ya 35' katika mchezo huo. Yanga walipata penalti hiyo
kufuatia mlinzi wa Mtibwa, Lundenga 'kuunawa' mpira akiwa ndani ya eneo la
hatari wakati akijaribu kuzuia mpira uliopigwa na mshambulizi wa Yanga,
Mzambia, Obrey Chirwa.
Kwa matokeo hayo Yanga wameendelea kubaki
nafasi ya pili wakiwa na pointi 53, alama mbili nyuma ya vinara Simba huku
zikiwa zimesalia mechi sita tu kabla ya kumalizika kwa msimu.
No comments:
Post a Comment