TANGAZA NASI HAPA

Tuesday, 7 March 2017

TFF Cup: Chirwa apiga nne na kufunga ‘hat trick’ yake ya kwanza Yanga SC ikitinga robo fainali…

MSHAMBULIZI wa Obrey Chirwa amefunga 'hat trick' yake ya kwanza akiichezea Yanga SC leo Jumanne. Raia huyo wa Zambia alifunga magoli yake katika dakika za 23', 45' na 70', 90’ katika ushindi wa Yanga 5-1 Kiluvya United katika mchezo wa hatua ya 16 borb ya michuano ya FA Cup, pia ndiye mchezaji wa kwanza wa timu hiyo kufunga magoli matatu au zaidi katika game moja msimu huu.

Geofrey Mwashuiya alifunga goli la uongozi dakika ya 13' kisha Chirwa akafunga goli lake la kwanza. Edgar Charles alifunga goli la kufutia machoni upande wa Kiluvya dakika ya 41'. Dakika tano baada ya Chirwa kukamilisha 'hat trick' yake, kiungo mshambulizi Juma Mahadhi akafunga goli la tano dakika ya 75'.

Mabingwa hao watetezi wa michuano hiyo sasa wamefuzu kwa robo fainali na kuungana na timu za Mbao FC ya Mwanza, Madini FC ya Arusha, Simba SC na Azam FC za Dar es Salaam, Ndanda FC ya Mtwara na Tanzania Prisons ya Mbeya.

No comments:

Post a Comment