GOLI la mkwaju wa penalty lililofungwa na
kiungo-mshambulizi, Shiza Kichuya dakika nne kabla ya kumalizika kwa mchezo limeinusuru Simba SC kuambulia kichapo
mbele ya Mbeya City FC katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara uliopigwa katika
uwanja wa Taifa Dar es Salaam jioni hii.
Ditram Nchimbi ambaye alikuwa katika ubora wa juu licha ya
kupoteza nafasi kadhaa za wazi alifunga
goli la uongozi upande wa Mbeya City dakika ya 37’ baada ya kupiga kiki kali
iliyombabatiza mlinzi wa Ahmad Juma na kutinga wavuzi. Nchimbi alipokea pasi maridadi
ya kisigino iliyopigwa na kiungo mshambulizi, Raphael kabla ya kufunga.
Mshambulizi, Ibrahim Ajib aliisawazishia Simba dakika ya 65’
kwa mkwaju wa faulo kufuatia kiungo Mohamed Ibrahim kuangushwa karibu na
eneo la mita 18.
Pasi za ‘One-Two’ kati ya nahodha wa City, Kenny Ally na Raphael
Breyson , kasha Nchimbi kupiga pasi maridadi ya mwisho ilizaa goli la pili
dakika ya 78’ mfungaji akiwa Kenny. Nchimbi angeweza kufunga goli la tatu
dakika ya 85’ baada ya kubaki yeye na kipa Daniel Agyei lakini umakini mdogo
ukamnyima nafasi ya kufunga.
Baada ya kukoswa goli la tatu Simba walifanya shambulizi la
kustukiza ambalo lilizaa mkwaju wa penalty kufuatia kuangushwa ndani ya eneo la
hatari kwa mlinzi wa pembeni Mohamed Hussein ‘Zimbwe Jr’ dakika ya 86’ na
Kichuya akaukwamisha mpira nyavuni na kufikisha goli lake la 11 msimu huu. Penalti hiyo ililalamikiwa sana na
wachezaji wa City.
Kutokana na matokeo hayo Simba imeendelea kubaki kileleni
mwa msimamo huku wakiwa na alama 55, ikiwa Yanga wataishinda Mtibwa siku ya
kesho watapanda juu ya msimamo kutokana na wastani wao mzuri wa magoli ya
kufunga na kufungwa.
No comments:
Post a Comment