IKICHEZA ugenini WWK Arena ‘wabishi’ RasenBallsport Leipzig
wamevutwa shati baada ya kulazimishwa sare ya kufunganga 2-2 na Augsburg mchezo uliopigwa usiku wa Ijumaa.
Konstantinos Stafylidis aliwafungia
wenyeji goli la uongozi dakika ya 19’,lakini goli hilo lilidumu kwa dakika sita
tu kabla ya kusawazishwa na mshambulizi, Timo
Werne. Timuhizo zilikwenda mapumziko zkiwa sare ya kufungana 1-1.
Marvin Compper
akaongeza goli la pili upande wa wageni dakika ya 52’, kabla ya Martin Hinteregger kusawazisha
dakika ya 60 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya kufungana 2-2.
Ligi hiyo
ya Ujerumani itaendelea leo Jumamosi kwa michezo sita kupigwa katika viwanja
tofauti huku mchezo kati ya Borussia Dortimund na Bayer Leverkusen katika
uwanja wa Iduna Park ukitaraji kutazamwa na wengi.
Ratiba kamili
ya mechi za leo ni kama ifuatavyo
16:30 Borussia Dortmund ? - ? Bayer
Leverkusen
16:30 FC Cologne ? - ? Bayern
Munich
16:30 Hoffenheim ? - ? Ingolstadt
16:30 Mainz 05 ? - ? Wolfsburg
16:30 Werder Bremen ? - ? Darmstadt
19:30 Borussia Moenchengladbach ? - ? Schalke
04
No comments:
Post a Comment