MSHAMBULIZI na nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa
Stars,Mbwana Samata usiku wa Alhamis alifanikiwa kufunga magoli mawili na
kuisaidia timu yake ya KRC Genk kuifunga KAA Gent 5-2 katika mchezo wa kwanza
ugenini hatua ya 16 bora katika michuano ya Europa League.
Malinovsky alianza kuifungia Genk goli la kwanza kwa shuti
la mpira faulo nje kidogo ya eneo la
hatari, wenyeji wakasawazisha goli hilo
kupitia kwa Samuel Kalu dakika ya 27.
Dakika ya 33 Omary Colley akaifungia Genk bao la pili
akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona uliopigwa kwa mguu wa kushoto na
Malinovsky. Dakika nne kabla ya mapumziko Samata akafunga akiwa ndani ya
eneo la hatari, ksha Jere Uronen akafunga la nne dakika ya mwisho ya kipindi
cha kwanza na kuifanya Genk kwenda
mapumziko wakiwa mbele kwa mabao 4-1.
Dakika 16 kabla ya kumalizika kwa mchezo Samata akafunga
goli la tano na kuifanya Genk kuondoka ugenini na hazina kubwa ya magoli kwani watatakiwa kufungwa 4-0 katika mchezo
wa nyumbani wiki ijayo ili kuondolewa katika michuano. Je, watafuzu kwa robo
fainali?
No comments:
Post a Comment