Mshambuli RAIA WA Hispania, Fernando Torres anaendelea
vizuri baada ya kuanguka na kuumia kichwa wakati wa mchezo wa ligi kuu ya
Hispania kati ya Deportivo La Coruna na AtleticoMadrid. Kwa mujibu wa ripoti ya
daktari mshambulizi huyo wa zamani wa Liverpool, Chelsea na Ac Milan hajapata
matatizo yoyote ndani ya kichwa.
Torres alianguka vibaya na kufikia kichwa baada ya kuruka
juu kuwania mpira dakika ya 85’ katika tukio ambalo lilizua hofu kubwa katika
uwanja wa Riazor. Huduma nzuri ya kwanza aliyopata kutoka kwa madaktari
uwanjani hapondiyo ilisaidia kuokoa maisha ya mshambulizi huyo.
Kupitia mtandao wa
klabu ya Atletico Madrid umeripoti kuwa Torres anaendelea vizuri hospitali na
anataraji kurejea uwanjani haraka.
No comments:
Post a Comment