VILABU
vikubwa barani ulaya vinamtolea macho mshambulizi wa Torino Andrea Belotti
ambaye alifunga magoli matatu 'Hat trick' katika ushindi wa 3-1 ambao Torino waliupata
siku ya jana Jumapili dhidi ya Palermo katika ligi kuu ya Italia 'Serie A.'
Chelsea
chini ya kocha Mtaliano, Antonio Conte, Manchester United, Arsenal, FC Bayern
Munich, Borussi Dortimund ni baadhi ya timu kubwa za ulaya ambazo zinapendezwa
na mshambuliaji huyo kijana aliyefunga magoli 21 msimu huu katika Serie A.
Belotti
ametokea wapi?
01:
Alizaliwa Disemba 20, 1993 katika mji wa Caccinate, huko Italia. Ana umri wa
miaka 23 hivi sasa.
02:
Akiwa na miaka kumi alijiunga na timu ya vijana ya Grumellese. Kati ya mwaka
2003 hadi 2006 alidumu katika timu hiyo kisha akahamia Albino Leffe hadi mwaka
2012.
03:
Alipandishwa katika kikosi cha wakubwa msimu wa 2012/13 na kufunga magoli 14
katika michezo 37 aliyoichezea AlbinoLeffe.
04: Agosti 2013 alijiunga na Palermo kwa mkataba wa mkopo akitokea Albino
Leffe kabla ya kununuliwa kwa usajili wa kudumu Julai 2014.
05: Septemba 24, 2014 alifunga goli lake la kwanza katika Serie A wakati
Palermo ilipotoka sare ya 3-3 dhidi ya Napoli. Belotti alifunga magoli mawili
katika mchezo huo.
06: Alifunga jumla ya magoli 16 katika michezo 62 aliyoichezea Palerm
07: Agosti 18, 2016 Belotti alijiunga na Torino kwa ada ya euro 7.5
milioni. Novemba 28 akafunga goli lake la kwanza katika Serie A akiichezea
Torino katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Bologna.
08: Baada yb kufanya vizuri msimu huu, Disemba 4, 2016, Belotti aliongeza
mkataba wa kuendelea kuichezea Torino hadi mwaka 2021 huku kukiwa na
kipengele cha kumruhusu kujiunga na timu
nyingine itakayofikb na dau lisilopungua euro milioni 100 kwa klabu za nje ya Italia.
09: Machi 5, 2017 Belotti alitumia dakika nane kufunga magoli matatu ' hat
trick' dhidi ya timu yake ya zamani Palermo na kufikisha magoli 20 katika
Serie. Sasa anafukuzia relodi ya Benjamin Santos ambaye alifunga magoli 27 katika msimu wa 1949/50 akiwa klabuni Torino.
10: Belotti amezichezea timu za Taifa za vijana za Italia, alifunga
magoli mawili katika michezo 6 aliyoichezea Italia U19, akafunga magoli manne
katika michezo tisa aliyoichezea Italia U20, akafunga magoli 9 katika michezo
18 aliyoichezea Italia U21.
Agosti 27, 2016 aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha timu ya
wakubwa ya Italia chini ya kocha Gian Piero Ventura kwa ajili ya mchezo wa
kirafiki vs Ufaransa.
Alifunga goli la kwanza akiichezea Italia katika ushindi wa 3-2 ugenini dhidi ya Macedonia Oktoba 9 katika mchezo wa kuwania nafasi ya
kufuzu kwa fainali za kombe la dunia 2018.
Hadi sasa ameichezea Azurri michezo mitano na kufunga magoli matatu.
Makala haya yameandaliwa na Baraka Mbolembole
No comments:
Post a Comment