TANGAZA NASI HAPA

Friday, 3 March 2017

Yanga SC kuifuata Mtibwa Sugar kesho…..




MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, timu ya Yanga SC inataraji kuondoka jijini Dar es Salaam  mapema asubuhi ya Jumamosi kuelekea mkoani Morogoro ambako watacheza na Mtibwa Sugar FC katika uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Katibu mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwassa amethibisha hilo. Yanga itacheza na Mtibwa katika mchezo wa 24 msimu huu, hadi sasa wapo nafasi ya pili nyuma ya Simba kwa tofauti ya pointi mbili baada ya kukusanya alama 52 katika michezo 23 waliyokwishacheza.

“ Leo ni siku ya pili vijana wanaendelea na mazoezi toka mchezo uliopita tuliocheza dhidi ya Ruvu Shooting, muda mfupi ujao wataingia tena mazoezini kisha watarejea kambini tayari kwa safari ya kesho asubuhi kuelekea Morogoro kwa usafiri wa basi la timu.” anasema Kwassa

"Kesho pia watafanya mazoezi pamoja na kuuzoea uwanja wa Jamhuri ambao utatumika siku ya mchezo (jumapili) dhidi ya Mtibwa, kama utawala tutahakikisha kila kitu kinaenda sawa ni pamoja na kuaandaa fungu la fedha kulipia gharama zote mkoani humo ili kuepuka kuingia madeni."

No comments:

Post a Comment