WAKATI wapinzani wao Zanaco FC kutoka Zambia wakitaraji
kuingia nchi saa kumi jioni leo Alhamis wachezaji Donald Ngoma, Amis Tambwe,
Juma Abdul,Thaban Kamusoko wote wameanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa
Jumamosi hii katika Caf Champions league.
Awali wachezaji hao walizua hofu ya kuukosa mchezohuo wa
kwanza hatua ya mwisho kabla ya kufuzu kwa hatua ya makundi kutokana na
majeraha yaliyokuwa yakiwakabili. Daktari wa Yanga SC, Dk. Babu amethibisha kuwa wachezaji hao
wanaweza kucheza mchezo huo isipokuwa mlinda mlango Beno Kakolanya na beki Pato
Ngonyani pekee.
“ Wachezaji wote
waliokuwa na majeraha wameshaanza mazoezi Jumatano hii,isipokuwa wachezaji
wawili Beno Kakolanya na Pato Ngonyani ambaye alikuwa na maralia na wanaendelea
na matibabu lakini wengine wote wameshaanza mazoezi. Mashabiki wa Yanga waondoe
wasiwasi kwa sababu Tambwe,Ngoma na Kamusoko wote wapo vizuri na wanaweza
kutumika katika mchezo wa Jumamosi ikiwa watapewa nafasi na benchi la ufunzi.” Anasema
Dk. Babu
No comments:
Post a Comment