Mshambulizi wa Gabon, Pierre-Emerick Aubemayang alifunga
magoli matatu ‘hat trick’na kuisaidia Borussia Dortimund kufuzu kwa robo
fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa ulaya. Kwa jumla ya magoli 4-1 dhidi ya
Benfica ya Ureno.
Aubameyang alifunga goli la kwanza dakika ya 4’ akimalizia
pasi ya Christian Pulisic.hadi mapumzikio BVB walikuwa mbele kwa goli 1-0.
Pulisic akaongeza goli la pili dakika 59’,kabla ya Aubameyang kufunga
magolimengine mawili dakika za 61’ na 85’ na kuisaidia timu yake kufuzu kwa
robo fainali sambamba na timuza FC Bayern Munich, Real Madrid na Barcelona.
No comments:
Post a Comment