MAGOLI ya Jon Bautista
6’, na Xabier Prieto 26’, 72’ yametosha
kuwapa ushindi muhimu ugenini Estadio Benito Villamarin timu ya Real Sociedad
baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 3-2 dhidi ya wenyeji Real Betis katika
mchezo wa ligi kuu Hispania-La Liga uliopigwa usiku wa Ijumaa.
Magoli ya Betis yalifungwa na Aissa
Mandi 16’, na Antonio Sanabria 65’. Ushindi
huo umewapeleka Sociedad hadi nafasi ya nne
katika msimamo wakiwa na alama 48-pointi mbili zaidi ya Atletico Madrid.
Ligi hiyo itaendelea kwa michezo huku vigogo FC Barcelona na
Real Madrid pia wakishuka viwanjani. Hii hapa ratiba kamili ya game za leo
Jumamosi.
14:00 Leganes ? - ? Granada
17:15 Eibar ? - ? Real
Madrid
19:30 Villarreal ? - ? Espanyol
21:45 Barcelona ? - ? Celta
Vigo
No comments:
Post a Comment