TANGAZA NASI HAPA

Thursday, 2 March 2017

Huku wakisubiri rufaa ya Chirwa, Ngoma, Tambwe kuwakosa Mtibwa Sugar…..




Na Baraka Mbolembole


MABINGWA watetezi wa ligi kuu Tanzania Bara,timu ya Yanga SC imeendelea  na mazoezi  yake  kujiwinda  na  mchezo dhidi  ya Mtibwa Sugar ambao  utapigwa siku  ya Jumapili hii katika uwanja  wa  Jamhuri, Morogoro.

Kuelekea  mchezo  huo mgumu,kikosi  hicho kilicho chini ya makocha  Mzambia, George  Lwandamina na  msaidizi  wake  Juma  Mwambusi  kinakabiliwa na  changamoto  kubwa  ya  majeraha  hasa  katika  eneo  la  ushambuliaji.
 Ikiwa  tayari  imekata  rufaa  kupinga  kadi  nyekundu aliyooneshwa  mshambulizi  wake  Obrey  Chirwa  katika mchezo  wa  ushindi  wa 2-0 dhidi  ya  Ruvu  Shooting  Jumatano  iliyopita hadi  sasa  Yanga  haina  uhakika  wa  kumtumia  mshambuliaji  yoyote  yule  wa  kigeni  kati  ya  washambuaji watatu  waliofunga  jumla  ya  magoli 25.
Mzimbabwe, Donald  Ngoma anaendelea  kuuguza  majeraha  yake  ya  goti  aliyopata  mwezi  Januari, Mrundi, Amis  Tambwe  alishindwa  kufanya  mazoezi  siku  ya  Alhamis  kutokana  na  maumivu  ya  goti, huku suala  la  rufaa  ya  Chirwa  likisubiriwa kutolewa  uamuzi na  Shirikisho  la  soka  nchini TFF  kupitia  Bodi  ya  ligi, huenda  washambuaji  wazawa, Emmanuel  Martin na Matheo Anthony wakapewa  nafasi  katika  mchezo  huo.
 
 Tumeendeleana  mazoeizi  Alhamis hii kujiwinda  na  mchezo  ujao  dhidi  ya  Mtibwa utaofanyika Morogoro, tunashukuru wachezaji wako  katika  hali nzuri, majeruhi  ni  wachache, kuna  Juma  Abdul ambayeambaye  anasumbuliwa na kifundo cha mguu, Donald  Ngoma kama  mnavyojua  bado  hajapona.”
 
“ Amis  Tambwe hatuji kama  anaweza  kucheza katika mechi  inayokuja. Tambwe  ana tatizo katika goti na alianza  kusikia  maumivu  mara  baada ya kumalizika  kwa mchezo dhidi  ya  Ruvu  na  Leo ( Alhamis) ameshindwa kufanya  mazoezi  vizuri hivyo  tunategemea  ripoti  maalumu kutoka kwa  daktari  ili  kujua  hali  yake.” Anasema kocha  msaidizi  wa  kikosi  hicho  Juma Mwambusi

No comments:

Post a Comment