TANGAZA NASI HAPA

Tuesday, 28 February 2017

Tegete na wachezaji wengine walivyotetea kiwango cha Juma Abdul hivi sasa





Na  Baraka  Mbolembole

WACHEZAJI  wa zamani  na  sasa  wameungana  kutetea  kiwango  cha baadhi  ya  wachezaji  wa  Yanga  SC  dhidi  ya  mahasimu  wao  Simba  SC  siku  ya  Jumamosi  iliyopita. Upande  wangu  sikuvutiwa  na  kiwango  cha  mlinzi  wa  kulia  wa  Yanga, Juma  Abdul  kwa  kuzingatia  uwezo  wake  wa  msimu  uliopita  na jinsi  anavyocheza  sasa.

 Mimi  nina  imani na  Juma Abdul  kwasababu  ameshapevuka kimpira, changamoto  na  mambo  ya  soka anayajua  vizuri hivyo  suala la  kurudisha  uwezo wake  wa  awali lipo ndani  ya  uwezo  wake, tumpe muda na  siyo  kumuhukumu.”  Anasema  nahodha  wa  Polisi  Moro  FC, Nahoda  Bakari.

“ Kisa  mechi ya  Jumamosi ndiyo  Juma  alaumiwe? Siku  zote  mlikuwa  wapi ‘kuwajaji’ . kubalini kufungwa hiyo  ndiyo  mechi  ya ‘derby’ hata  Kessy  angecheza kwa  mfano na timu  ingefungwa  wangesema  kwa  sababu  katoka  Simba. Tutajaribu kuangalia  mbali sio  hapa. Tabu  yetu Watanzania ni  kulaumu  tu  ndiyo maana  soka  letu  haliendelei milele.” Anasema mshambulizi  wa  zamani  wa  Yanga, Jerson  Tegete  ambaye  sasa  anaichezea  Mwadui  FC ya  Shinyanga.
“ Mchezaji  huwezi  kudumu moja  kwa  moja katika  kiwango, hata  ulaya  tunaona  wakati  mwingine  wachezaji  wanashindwa itakuwa  hapa  Bongo ambako mnaweza  kukaa miezi  mitatu bila  kulipwa mshahara. Huyo  Juma  kiwango  kimeshuka  lini  au  juzi baada  ya  kufungwa na  Simba?” anahoji  Tegete  mmoja  kati  ya  wafungaji  bora  watatu  wa  muda  wote  katika  ‘Dar-Pacha’

“ Mchezaji ana changamoto kam umecheza ama unacheza mpira utaelewa. Kwa  hapa  Bongo mchezaji anapofanikiwa kulinda  kiwango  chake  walau  kwa miaka  mitano  anastahili pongeza hasa  kwa  kizazi  cha  sasa. “

Mchezaji  anasafiri  kucheza  mechi Bukoba  mpaka  Songea, Mtwara  mpaka  Mwanza na  mshabiki  anataka  kiwango kilekile wakati  viwanja  ni  vibovu, malipo ‘kiduchu’ huku nyumbani familia  ina  matatizo. Kila mechi ina falsafa iliyommeza,tujifunze Mpira.” Anasema kipa  wa  zamani  wa  timu  za Taifa  za  Tanzania  na  klabu  ya Polisi  Morogoro,Madopi  Mwingira  amuunga  mkono Tegete.

“ Ni  kweli  kaka  Madopi, sema  hawajui,ndiyo  maana wanaona  watu wakiwa Simba, Yanga,Manchester  United, Real Madrid hawajui  kuwa  muda  mwingine kuna  mambo  yanakuwa  yakiendelea ndani  ya  klabu. Hatukatai mechi  za  Simba  na  Yanga  kuwa  zinaleta  mawazo sana kutokana  na  ushabiki, lakini tubakize  maneno ya  akiba siyo  kisa  timu  yako  imefungwa basi  utoe  yote.” Anasisitiza  Tegete  ambaye  ameshafunga  magoli  matano  katika  mipambano  ya  Yanga  na  Simba.

“ Mimi  nimecheza  muda  mrefu ligi  ya  Bongo pamoja  na  timu  ya  Taifa, na  sasa  nimeusoma mpira, tujadili  kama  ‘wajuzi’. Simba na  Yanga  ni  kipimo  kizuri kwa  mchezaji  na  timu. Ili mpira uendelee ikiwemo  viwango  vya  wachezaji, haya ndiyo  mambo  muhimu. Moja, ufundi, Pili, waamuzi bora, Tatu, uongozi mathubuti, Nne, wadau, na  Tano  matibabu mazuri. Mimi  nadhani  namba  moja  ndiyo  tuangalie, pia  makocha, tujifunze  soka.” Anasema  Madopi na  kuongeza.
 “ Kwa  mfano, nimzungumzie  Vicent  Andrew ‘Dante’, goli  lililofungwa  na  Laudit  Mavugo, mjuzi  anajua  na  ameona  beki anaangalia kushoto , mshambuliaji yupo nyuma anafnga. Kwangu Danteni miongoni  mwa mabeki bora  wanaochipukia, kiufundi  mchezaji  anatakiwa aangalie  mpira, sehemu  iliyowazi  na  mpinzani  wake. Hapa ndiyo  ufundi  sasa  unahitajika, kuna  principle of  attacks and  defence. Mpira ni  kuzuia na  kushambulia.”
  
“ Madopi  Mwingira, Jerson  Tegete mmetumia vipaji  vyenu juu  ya  soka kumfahamisha kidogo mchambuzi Baraka Mbolembole,nashukuru amewaelewa. Uchambuzi  wa  mpira wa  miguu unahitaji uelewa wa  mpira, uwe  mchezaji, uwe  kocha, daktari, meneja, na  waandishi wa  habari  za  michezo. Umefika  wakati  tuendane  na  wakatisiyo  ‘blablaa’ hiyo  ni  kazi  ya  muda  mfupi zaidi  duniani, imejaa  mizengwe, fitna  na  majungu.” Anasema  mchezaji  nyota  wa  zamani  wa  Taifa  Stars, Athumani  Jumapili  Chama.

“uchambuzi wa mpira wa miguu unaitaji uelewa wa mpira,uwe mchezaji,coach,dk team,meneja team na wahadishi wa michezo hao wana ueledi,uelewa wa football,imefika wakati tuendane na wakati,sio blablaa ndo kazi ya muda mfupi zaidi duniani,imejaa mizengwe,fitna,majungu

No comments:

Post a Comment