TANGAZA NASI HAPA

Tuesday, 28 February 2017

CHAMPIONSHIP; Newcasstle yatumia dakika tisa kurejea kileleni, yaipiga Brighton




NEWCASTLLE  walitumia  dakika tisa  za  mwisho  kutoka  nyuma 1-0  na  kuibuka  na  ushindi  muhimu  dhidi  ya Brighton na  ‘kukwea’  kileleni  mwa  msimamo  wa  ligi  daraja  la  kwanza –Championship  kwa  tofauti  ya  pointi  mbili.

Mshambulizi ‘veterani’  Glenn Murray  alifunga  kwa  mkwaju wa  penalty  dakika  ya 14  na  kuwapa  wenyeji  uongozi  ambao  uliwafanya  kuwa  mbele  kwa  pointi  nne  dhidi  ya  Newcastle. 

Mohamed  Diame alisawazisha  goli  hilo  dakika  ya  81’,  na Ayoze Perez  akapiga la  ushindi  dakika  moja  kabla  ya  kumalizika  kwa  mchezo  na  kuwapa  ushindi  wa  2-1  vijana  wa  kocha  Rafael Benitez

MATOKEO  YA  MICHEZO MINGINE  YA  USIKU  WA  JUMANNE
FT Aston Villa 2 - 0  Bristol City
FT Blackburn Rovers 1 - 0  Derby County

FT Brighton & Hove Albion 1 - 2  Newcastle United

No comments:

Post a Comment