IKICHEZA nyumbani,
Geusseppe Meazza, timu ya
Inter Milan ilikubali
kipigo cha mabao
3-1 kutoka kwa
AS Roma katika
mchezo wa ligi kuu ya
Italia Serie A. Kiungo, Radja Nainggolan alifunga mara
mbili katika dakika
za 12’ na 56’ kabla ya nahodha
wa Inter, Mauro Icardi kufunga goli
la kufutia machozi
dakika ya 81’.
Diego Perotti
aliifungia Roma goli
la tatu kwa
mkwaju wa penalty zikiwa
zimesalia dakika tano mchezo
kumalizika na kuendelea
kuwafukuza mabingwa mara
nne mfululizo Juventus ambao waliibuka
na ushindi wa 2-0 siku
ya Jumamosi dhidi ya
Empoli. Juventus wanaongoza ligi
kwa tofauti ya
pointi Saba huku zikiwa zimesalia
mechi kumi kabla
ya kumalizika kwa msimu
Juve wamekusanya alama
66, Roma wana pointi 59 huku SS Napoli
ambao walichapwa 2-0 nyumbani
na Atalanta wanashika nasfasi
ya tatu wakiwa na
alama 54. Ligi hiyo
itaendelea tena usiku wa
Jumatatu hii kwa
Fiorentina kuwakaribisha Torino.
HAYA HAPA
MATOKEO YOTE YA
SERIE A MZUNGUKO WA 26
February 25
FT SSC Napoli 0 - 2 Atalanta
FT Juventus 2 - 0 Empoli
February 26
FT Palermo 1 - 1 Sampdoria
FT ChievoVerona 2 - 0 Pescara
FT Crotone 1 - 2 Cagliari
FT Genoa 1 - 1 Bologna
FT Lazio 1 - 0 Udinese
FT Sassuolo 0 - 1 AC
Milan
FT Inter 1 - 3 Roma
February 27
21:45 Fiorentina ? - ? Torino
No comments:
Post a Comment