TANGAZA NASI HAPA

Monday, 27 February 2017

Mtibwa Sugar vs Yanga SC kupigwa Jamhuri Stadium





 SHIRIKISHO la  Soka nchini-TFF  limeufungulia  uwanja  wa  Jamhuri,Morogoro  kwa  matumizi  yamichezo  ya  ligi  kuu  Tanzania  Bara msimu  unaoendelea.


Uwanja huo  ulifungiwa  kwa muda usiojulikana  mapema mwezi  Januari  mara  baada  ya  mchezo  wa ligi  kuu  kati  ya  wenyeji  Mtibwa  Sugar  dhidi  ya  Simba  SC kutokana  na  ubovu  wa  eneo  la  kuchezea-pitch.


TFF iliufungia Uwanja wa Jamhuri ili kutoa fursa kwa wamiliki wake kuufanya marekebisho makubwa kwenye eneo la kuchezea huku askari polisi kupata maelekezo ya kutosha ya jinsi ya kusimamia usalama uwanjani badala ya kutazama mechi. 


 Kwa  maana  hiyo  mchezo  wa  Machi 5  kati  ya  Mtibwa  na mabingwa  watetezi  Yanga  SC  utachezwa  katika uwanja  huo uliopo  katikati  ya  mji  wa  Morogoro baada ya  Chama  cha  Soka  Manispaa  ya  Morogoro  na  wamiliki  wa uwanja  huo  kufanya  jitihada  kubwa  kurekebisha  mapungufu  yaliyokuwepo  awali.




PICHA  kwa  hisani  ya  Dastan  Shekidele 

No comments:

Post a Comment