IKICHEZA nyumbani Stade Orange Velodrome, timu ya
Olympique Marseille ilikubali
kipigo ‘kizito’ kutoka
kwa PSG. Mlinzi wa kati, Mbrazil, Marquinhos alifungua ‘karamu’ ya
magoli dakika ya 6’,
kisha Edson Cavanni dakika kumi baadae akafunga goli
lake la 26
katika Ligue 1 msimu huu.
Mabingwa hao
watetezi walikwenda
mapumziki wakiwa mbele
kwa magoli 2-0. Lucas Moura
alifunga goli la
tatu dakika ya 50’, Mjerumani, Julian Draxler akaongeza linguine dakika
ya 61’ na kufanya
matokeo kuwa 4-0.
DEPAY APIGA MBILI
LYON IKIUA 5-0
Kiungo mshambuliaji
aliyeshindwa kutamba Manchester
United,Mholland, Memphis Depay
ameendelea kufurahia uhamisho
wake wa kujiunga na Olympic Lyon ya
Ufaransa mwezi Januari. Depay alifanikiwa
kufunga magoli mawili katika
ushindi wa 5-0 dhidi
ya Metz.
Alifunga dakika za 43’,
53’, na
kumtengenezea goli Alexandre Lacazette dakika ya 78’.
Magoli mengine ya
mabingwa hao mara
saba mfululizo wa
zamani yalifungwa na Ivan
Balliu ambaye alijifunga dakika
ya 74 na Mathieu
Valbuena aliyefunga dakika ya
mwisho kabisa ya
mchezo.
MATOKEO YOTE YA
LIGUE 1 WIKENDI JANA HAYA HAPA
February 24
FT Nantes 3 - 1 Dijon
FT Nice 2 - 1 Montpellier
February 25
FT Guingamp 1 - 2 Monaco
FT Angers 3 - 0 SC
Bastia
FT Lille 2 - 3 Bordeaux
FT Nancy 0 - 0 Toulouse
FT Rennes 1 - 0 Lorient
February 26
FT Saint-Etienne 0 - 1 Caen
FT Lyon 5 - 0 Metz
FT Marseille 1 - 5 Paris
Saint Germain
No comments:
Post a Comment