JUVENTUS ilitoka nyuma 1-0 na kufunga magoli
matatu kipindi cha
pili na kuifunga
SSC Napoli 3-1 katika
mchezo wa nusu
fainali ya kwanza ya
Coppa Italia usiku
wa Jumanne hii
katika uwanja waJuventus,
Turin.
Jose Maria Callejon
aliwapa Napoli uongozi
wa mchezo dakika ya 36’
huku kipa Pepe
Reina akifanya kazi nzuri kipindi
cha kwanza kwa
kuzuia nafasi nyingi
za magoli kutoka
kwa Paulo Dyabala
na Gonzalo Higuain.
Dakika ya 13’,
Reina alizuia mpira
wa kichwa uliopigwa
na Mario Mandzukic , nusu
saa baadae Reina alifuta
nafasi ya wazi
ya Kwadwo Asamoah.
Pasi za ‘One-Two’
kati ya Lorenzo
Insigne na Arkadiusz Millik zilitengeneza
nafasi ya kupatika
goli pekee la
Napoli dakika tisa kabla ya
mapumziko.
Paulo Dyabala
alifunga kwa penalty dakika mbili baada
ya kuanza kwa
kipindi cha pili
baada ya kuchezewa
vibaya na mlinzi
wa Napoli Kalidou Koulibaly. Mshambulizi wa
zamani wa Napoli,
Muargentina, Gonzalo Huguain alifunga goli
la pili dakika ya 64’.
Dybala akafunga goli
la tatu kwa
mkwaju wa penalty dakika
ya 69’ na kuihakikishia
Juventus ushindi wa 3-1 katika
nusu fainali ya
kwanza.
No comments:
Post a Comment