TANGAZA NASI HAPA

Tuesday, 28 February 2017

Brighton vs Newcastle ; Ni ‘fainali’ kupanda EPL, vita ya Chris Hughton na Rafa Benitez Leo….





 BRIGHTON& Hove Albion itaikaribisha  Newcaste  United  katika  dimba  la The American Express Community usiku  wa  Leo  katika  mchezo  muhimu  wa  ligi  daraja  la  kwanza  England ‘Championship’.

Timu hizo mbili zimekuwa na  msimu mzuri  katika  Championship  na  mara  kwa  mara  zimekuwa  zikiteremshana  kileleni. Brighton & Hove Albion inaongoza  msimamo  hadi  sasa  ikiwa  na  alama  71 baada  ya  kucheza  michezo 33 huku  Newcastle  ikifuatia  ikiwa  na  pointi 70  baada  ya  kushuka  dimbani  mara 33 pia.
Mchezo  wao  wa  kwanza  msimu  huu Mwezi  Agosti, 2016  kikosi  cha  kocha  RafaeL  Benitez  kilifanikiwa kuchomoza  na  ushindi  wa  magoli 2-0  katika  uwanja  wa St.James Park, shukrani  kwa  magoli  ya Jamaal Lescells 15’,  na Jonjo  Shelvey 63’ lakini  tangu  wakati  huo  kikosi  cha  Chris  Hughton  kimeimarika  na  sasa kinawania  nafasi ya kupanda ligi kuu msimu  ujao  kama  mabingwa.

Timu hizo zimekutana  mara  tatu na  mara  mbili  ambazo ‘Toon’  wamekwenda The  American  Express  hawajawahi kushinda. Januari 28, 2012 Brighton  iliichapa  Newcastle 1-0  na  kuwaondoa  katika  michuano  ya  FA  Cup, Januari 5, 2013  Newcastle  ililala  tena  2-0 na kuondolewa  katika  michuano  ya  FA.
Kocha wa  Brighton, Hughton  aliwahi  kuisimamia  Newcastle  na  kuipandisha  ligi  kuu  msimu  wa  2009/10  na  sasa  anaweza  kufanya  hivyo  kwa  mara  nyingine   akiwa  na  kikosi  hicho  cha  Brighton msimu  huu.

Mshambulizi  mwenye  miaka  27, Dwight Gayle amefunga  magoli  20  katika  michezo  24 aliyoichezea Newcastle  katika  Championship na ndiye  kinara wa  magoli  katika  ligi  hiyo. 

Glenn Murray ‘babu’ mwenye  umri  wa  miaka 33  amekuwa  mfungaji  kiongozi  wa  Brighton msimu  huu akifunga  magoli  16  katika  michezo  33. Nani  ataibeba  timu  yake  Leo? Tusubiri  na  kuona.


MECHI  ZA  LEO  JUMANNE  KATIKA  CHAMPIONSHIP

21:45 Aston Villa ? - ?  Bristol City

21:45 Blackburn Rovers ? - ?  Derby County

21:45 Brighton & Hove Albion ? - ?  Newcastle United

No comments:

Post a Comment