REAL Sociedad ililazimishwa
sare ya kufungana 2-2 nyumbani Estadio Anoeta
dhidi ya Eibar . Juanmi aliwafungia
wenyeji goli la
kuongoza dakika ya 14’.
Goli hilo lilidumu
kwa dakika 12 tu
baada ya Gonzalo Escalante kuisawazishia
Eibar dakika ya 26’.
Mchezo huo
ulikwenda mapumzik timu
hizo zikiwa sare
ya kufungana 1-1 na
mara baada ya
kuanza kwa kipindi
cha pili, kadi
mbili nyekundu zilitolewa.
Dakika ya Florian
Lejeune alioneshwa kadi ya
pili ya manjano
na kuondolewa uwanjani
upande wa Eibar, dakika
ya 59’, Juanmi wa
Real Sociedad naye
akaondolewa uwanjani kwa
kati ya pili
ya njano iliyoambatana
na ile nyekundu.
Mshambulizi wa
Mexico, Carlos Vela aliwafungia
Sociedad goli la pili
kwa mkwaju wa penalty na
huku ikionekana kama
wageni wamelala, dakika ya
tatu ya muda
wa nyongeza Pedro Leon akaisawazishia Eibar.
Katika mchezo mwingine
katika dimba la
Mestalla, wenyeji Valencia walishida
1-0 dhidi ya Leganes. Goli pekee
katika mchezo huo
lilifungwa na mlinzi Eliaquim
Mangala dakika ya 29’. Leganes
ilicheza pungufu mchezaji
mmoja kufuatia kadi
mbili za njano
alizooneshwa Alberto.
Ikicheza ugenini Estadio La Rosaleda, timu ya
Real Betis ilitoka
nyuma 1-0 na kuishinda
Malaga katika mchezo mwingine uliopigwa
usiku wa Jumanne. Pablo Fornals aliifungia Malaga
goli la uongozi
dakika ya 39’.
Jonas Martin aliisawazishia
Betis dakika ya 48’
na zikiwa zimesalia
dakika 16 mchezo kumalizika Antonio Sanabria akafunga
goli la ushindi
na kuwapa Betis
ushindi 2-1.
MECHI ZA LEO KATIKA
LA LIGA
FT Real Sociedad 2 - 2 Eibar
FT Malaga 1 - 2 Real
Betis
FT Valencia 1 - 0 Leganes
March 1
20:30 Barcelona ? - ? Sporting
Gijon
20:30 Osasuna ? - ? Villarreal
22:30 Celta Vigo ? - ? Espanyol
22:30 Granada ? - ? Alaves
22:30 Real Madrid ? - ? Las
Palmas
No comments:
Post a Comment