LEONEL Messi alifunga
goli lake la 20
msimu huu katika
ligi kuu ya
Hispania na kuisaidia
FC Barcelona kuibuka
na ushindi muhimu Estadio Vicente Calderondhidi ya
wenyeji Atletico Madrid.
Kiungo Mbrazil,
Rafinha aliifungia Barca
goli la uongozi
dakika ya 64’ kwa msaada
wa Luis Suarez
lakini goli hilo
lilidumu kwa dakika
sita tu kabla
ya mlinzi Diego Godin kusawazisha
dakika ya 70’
kwa msaada wa
kiungo , Koke.
Messi akafunga goli
la ushindi zikiwa
zimesailia dakika tatu
mchezo kumalizika na
kuifanya Barcelona kufikisha
alama 54 ambazo
ziliwapeleka kileleni kwa
muda kabla ya
Real Madrid kuwavaa
Villareal.
MORATA AIBEBA REAL
REAL Madrid walilazimika
kucheza ‘kufa na kupona’
ili kuepeka kipigo
cha tatu msimu
huu katika La Liga
baada ya kuwa
nyuma 2-0 dhidi
ya Villareal katika
dimba la Estadio de la Ceramica. Timu hizo
zilikwenda mapumziko zikiwa
suluhu-tasa na kufikia
dakika ya 56’ wenyeji
walikuwa mbele 2-0.
Manuel Trigueros alifunga
goli la kwanza
dakika ya 50’, Cedric Bakambu akaongeza la
pili dakika ya 56’
. baada
ya kufungwa magoli hayo
mawili kocha wa
Real, Zinedine Zidane
alimtoa kiungo wake
wa ulinzi Casemiro
na kumpa nafasi Isco dakika
ya 58’.
Mabadiliko hayo yalikuwa
na maana kwani
Gareth Bale alifunga
goli la kwanza
dakika ya 64’
kwa msaada wa
mlinzi Daniel Carvajal. Hilo ni
goli la pili
mfululizo kwa Bale
ambaye amerejea uwanjani
wiki iliyopita baada
ya kuuguza majeraha
kwa miezi mitatu.
Mwanasoka bora wa
dunia, Cristiano Ronaldo alifunga
goli lake la
16 msimu huu
katika La Liga
huku likiwa goli
la kusawazisha dakika
ya 74’.
CR7 alifunga goli
hilo kwa mkwaju
wa penalty. Pasi maridadi ya
mlinzi wa kushoto
Marcelo ilitumiwa vizuri
na Alvaro Morata ambaye
alifunga goli la
tatu zikiwa zimesalia
dakika saba mchezo kumaliziika
na kuirudisha Real
Madrid kileleni wakiwa na
pointi 55.
MATOKEO YOTE YA
LA LIGA WIKENDI
ILIYOPITA HAYA HAPA
February
24
FT Las Palmas 0 - 1 Real
Sociedad
February 25
FT Alaves 2 - 1 Valencia
FT Real Betis 1 - 2 Sevilla
FT Leganes 4 - 0 Deportivo
La Coruna
FT Eibar 3 - 0 Malaga
February 26
FT Espanyol 3 - 0 Osasuna
FT Atletico Madrid 1 - 2 Barcelona
FT Athletic Bilbao 3 - 1 Granada
FT Sporting Gijon 1 - 1 Celta
Vigo
FT Villarreal 2 - 3 Real
Madrid
|
No comments:
Post a Comment