TANGAZA NASI HAPA

Tuesday, 28 February 2017

‘Tunadaiwa, tutamlipa Vicent Bossou’-Mkwassa




 Na Baraka  Mbolembole

KATIBU  Mkuu  wa  klabu  ya Yanga  SC,Charles  Boniface  Mkwassa  amekiri  klabu  yake kudaiwa  na mlinzi  wa  kimataifa wa  Togo, Vicent Bossou.

Mlinzi  huyo  wa  kati  ilidaiwa  ni mgonjwa  wa nyonga  ndiyo maana  hakupangwa katika  mchezo  wa  kichapo  cha 2-1  kutoka  kwa  Simba SC siku  ya  Jumamosi  iliyopita, lakini  ukweli   mchezaji  huyo  wa  timu  ya Taifa  ya  Togo  aligomea  mchezo  huo  kwa madai  ya  kudai  mishahara  yake  ya  miezi  minne.

“ Nachofahamu  mimi  ni  kwamba  kuna mishahara  ya  mwezi  wa  nane ambayo  ilicheleweshwa, si  kwa  Bossou  tu  ni  timu nzima. Mshahara  wa  mwezi  wa  12  zikiwa  zimebaki  siku  kumi kila  mchezaji  aliandikiwa  cheki, wakalipwa  pamoja  na mshahara  wa  mwezi  wa  kwanza.” Anasema  Mkwassa 

 Kupitia  kurasa  ya  mtandao wake  wa  kijamii  Bossou  aliweka  wazi  kuwa hajalipwa  mshahara  wa miezi  minne  sasa  na  kuutaka  uongozi wake  kumlipa  haraka.

 Sasa  wakati  cheki  zinatoka, Bossou alikuwa alikuwa  kwenye  mashindano AFCON kule  Gabon na  yule  mtoa  cheki hakumkabidhi  mtu  yeyote  cheki  ya  mtu  mwingine  hadi  muhusika  mwenyewe awepo kwa  hiyo cheki  ya  Bossou  ilirudi  ofisini. “

 “ Alivyorejea tulimwambia  afuatilie  cheki  yake lakini  hakwenda na  tumejaribu  kufuatilia  tumeona  kuna  matatizo kidogo. Mshahara  wa  mwezi  wa  pili  kila  mchezaji  bado  hajapokea kama  unavyojua  timu  yetu ina  matatizo  kidogo kwa  mwenyekiti  hivyo mambo mengi  yamesimama.”


No comments:

Post a Comment