.
.
TANGAZA NASI HAPA
Monday, 13 March 2017
Hiki hapa kikosi cha kwanza cha Taifa Stars chini ya Mayanga
Kocha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ Salum Mayanga ametangaza majina 26 ya wachezaji watakaounda kikosi cha timu ya taifa kwa ajili ya maandalizi ya kufuzu kucheza michuano ya CHAN pamoja na ile ya AFCON.
Magolikipa: Aishi Manula (Azam), Deogratius Munishi ‘Dida’ (Yanga) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Mabeki: Shomary Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Yanga), Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba), Gadiel Michael (Azam), Andrew Vincent (Yanga), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba) na Erasto Nyoni (Azam FC).
Viungo: Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam), Said Ndemla (Simba), Frank Domayo (Azam), Muzamiru Yassin (Simba), Simon Msuva (Yanga), Shiza Kichuya (Simba), Farid Mussa (DC Tennerife) na Hassan Kabunda (Mwadui FC).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk, Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna, Sweden), Ibrahim Hajib (Simba), Mbarak Yussuf (Kagera Sugar) na Abdulrahman Mussa (Ruvu Shooting).
Stars itaingia kambini Machi 19 mjini Dar es Salaam na itacheza mechi mbili za kirafiki za kujipima nguvu.
Mechi hizo zitachezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Botswana Machi 25 na Burundi Machi 28.
Taifa Stars itaanza na Rwanda katika kuwania tiketi ya CHAN mwakani nchni Kenya na mechi ya kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam kati ya Julai 14 na 16 kabla ya timu hizo kurudiana Uwanja wa Amahoro, Kigali kati ya Julai 21 na 23.
Ikifanikiwa kuitoa Rwanda, Tanzania itamenyana na mshindi kati ya Uganda na ama Sudan Kusini au Somalia katika Raundi ya Tatu ya mchujo mechi ya kwanza ikichezwa kati ya Agosti 11, 12 na 13 na marudiano kati ya Agosti
Jicho la 3; Yanga 1-1 Zanaco, tatizo ni Lwandamina na mbinu zake mbovu, kutoamini vipaji vingine…
Na Baraka Mbolembole
HATA kabla ya mabadiliko ya kutoka na
kuingia Deus Kaseke dakika za mwisho tayari ‘nilishang’amua’ uwezo mdogo wa
kocha George Lwandamina.
Mkufunzi huyo mkuu wa Yanga SC raia wa
Zamabia sasa atahitaji kufanya
‘ushawishi’ mkubwa kwa mashabiki wa timu hiyo ili kumuamini kuwa ni ‘kocha
sahihi’ wa kuisogeza mbele timu bora iliyoachwa na mtangulizi wake
Mholland,Hans van der Pluijm.
Kila mtazamaji wa mchezo wa Jumamosi hiii
kati ya wenyeji Yanga dhidi ya Zanaco FC kutoka Zambia alifurahishwa na uwezo
wa juu ulioneshwa na kiungo mchezesha
timu wa Zanaco, Zimbseleni Moyo ambaye alitawala kiungo katika mchezo huo wa
kwanza hatua ya mwisho ya mtoano kuwania
kufuzu kwa makundi.
Kila ‘Mzalendo’ alitaraji matokeo bora kwa
wawakilishi hao wa Tanzania Bara,lakini wengi waliishia kulaumu kiwango cha
timu ndani ya uwanja na timu ya ushindi. Siku mbili kabla ya mechi niliandika
kwamba kocha wa Yanga, Lwandamina na
wasaidizi wanapaswa kuundaa ‘timu mpya ya mpito’ kutokana na wachezaji wengi
muhimu kuwa na majeraha.
Licha ya ‘kulazimishwa kucheza’ huku wakiwa
na maumivu Wazimbabwe, Donald Ngoma na
Thaban Kamusoko kikosi cha Yanga kilionekana kitakabaliwa na ‘mchezo mgumu’
katika uwanja wa nyumbani mbele ya mabingwa hao wa Zambia, huku habari za
wachezaji kupoteza morali kutokana na ukosefu wa mishahara zikiongeza wasiwasi
kama kweli timu iko tayari kwa mchezo huo muhimu.
Presha bila shaka ilikuwa kubwa kwa
Lwandamina,huku kuwakosa wachezaji wake Amis Tambwe,Haruna Niyonzima
kukimaanisha timu ‘itakosa makali’ katika ushambuliaji na ufungaji.
Bila Ngoma aliye katika makali, Yanga
ilianza mchezo ikiwa na mshambulizi mmoja, viungo wawawili wa pembeni ( Saimon
Msuva na Obrey Chirwa,) na viungo watatu katikati ya uwanja ( Kelvin Yondan,
Justine Zulu na Thaban.) Hassan Kessy na Mwinyi Hajji katika beki za
pembeni,nahodha Kelvin Yondan na Vicent Bossou katika ulinzi wa kati.
Katika benchi walikuwepo golikipa Ally
Mustapha, walinzi watatu Oscar Joshua, Juma Abdul, na Vicent Andrew, pia
walikuwepo viungo watatu wa mashambulizi, Deus Kaseke, Juma Mahadhi na Emmanuel
Martin ambao wote walipata nafasi ya kucheza kipindi cha pili.
Katika muda wote wa dakika 60’ alizokuwa
uwanjani,Ngoma alikuwa ‘mtu wa mashabiki’ wa Yanga na ‘hakubanduka midomoni
mwao’ hata pale alipotolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Mahadhi. Ngoma
alionekana ‘kupwaya’ katika mfumo ambao
ulimfanya acheze kama mshambulizi pekee, huku Kamusoko akicheza nyuma yake.
Alipokuwa akigusa mpira alionekana hayupo
‘fiti’na nafikiri hata kocha Lwandamina alikosea kumpanga mshambulizi huyo
pekee. Kwa kutambua majeraha aliyonayo,Lwandamina alipaswa kumpanga Ngoma
sambamba na Chirwa katika mfumo wa 4-4-2 ili kumsaidia mchezaji huyo
‘aliyejitolea kuccheza japokuwa hayupo tayari kimwili.’
Ndiyo,Ngoma alionresha kiwango cha
kufadhaisha sana lakini uwepo wake uwanjani uliisaidia Yanga kuwa salama kwa
sababu wachezaji wa Zanaco wanafahamu kuhusu makali yake katika ufungaji. Hivyo
hawakusogea kwenda mbele.
Upande wangu nitaendelea kumlaumu kocha
Lwandamina kwa sababu hakujiandaa kukabiliana na majeraha yanayoisumbua timu yake,na ni yeye ndiye
sababu ya kiwango kibovu cha timu. Wachezaji wengi wamekuwa wakilalamikia
nafasi wanazochezeshwa na kocha huyo,jambo ambalo limefanya washindwe kutoa
matokeo mazuri kama ilivyokuwa wakati wa Hans van der Pluijm.
Mfumo wa kumpanga Ngoma pekee wakati akiwa
na majeraha uliimaliza timu ndiyo maana mpira haukuwa ukikaa mbele walau kwa
dakika moja tu. Ndiyo wachezaji wanaweza kufanya vyema katika mfumo wowote,
lakini si rahisi ikiwa hawapo ‘fit’ kimwili na kiakili. Ngoma amecheza mara
kadhaa kama mshambulizi ‘huru’ wakati wa Hans na alifanya vizuri kwa sababu
alicheza akiwa bila maumivu.
Bahati mbaya kwa Lwandamina ni kwamba Ngoma
na Kamusoko walicheza pasipo kujiamini na wakati mechi ikiendelea wakaonekana
hadi na wapinzani wao kwamba hawako ‘fit’ Lwandamina alianza kupunguza makali
ya timu kutokana na mfumo wake na kutowaamini vijana wenye vipaji kama Hassan
Mhilu ambaye angeweza kufanya vizuri zaidi ya Kelvin Yondan ambaye alichezeshwa
namba sita.
Baada ya kipigo cha 4-0 kutoka kwa Azam FC
katika michuano ya Mapinduzi Cupmapema mwezi Januari nilianza kujenga hofu
kuhusu mbinu za Lwandamina,mechi mbili alizoisimamia Yanga vs Simba ( Mapinduzi
Cup na ligi kuu,) na baadaye suluhu-tasa dhidi ya Mtibwa sikuwana shaka tena
zaidi ya kuamini chini ya Mzambia huyu Yanga itapata wakati mgumu.
Sasa timu ambayo ilikuwa katika kiwango cha
juu kiuchezaji,hamasa,uwajibikaji imebadilika huku wachezaji wakiendelea
kushuka viwango kila leo. Kama wachezaji wanashuka viwango hii inamaanisha kuwa
uwezo wa kocha nimdogo.
Upande wangu ni mmoja kati ya
wanaohitajimatokeo bora,kocha kama huna uwezo wa kupanga kikosi na kufanya
mabadiliko basi ‘hukidhi’mahitaji ya timu. Lwandamina alipaswa kumuanzisha Deus
Kaseke au Mhilu katika wing mojawapo sambamba na Saimon Msuva huku Ngoma na
Chirwa wakicheza kama washambuliaji ‘wanaotegemeana.’
Unapokutana na timu iliyo bora katika
kiungo,kama ilivyokuwa kwa Zanaco alafu unamtoa mchezaji kama Kamusoko ambaye
alikuwa bora kuliko wote upande wako na kumuingiza Mahadhi ambaye hana uwezo
mkubwa wa kukaa katikati ya uwanja, ni dalili za kuwafanya watu waendelee
kuhoji kuhusu uwezo wa Lwandamina.
Inakuwaje aliingiza timu yake katika mfumo
wa kuzuia katika uwanja wa nyumbani? Lwandamina hakupaswa kujaribu mfumo katika
mechi muhimu,na alipaswa kumuweka benchi Kelvin au ili kutoa nafasi kwa
wachezaji asilia wa nafasi ya kiungo kuchukua mipira nyuma na kuipeleka mbele
jambo ambalo Kelvin alishindwa na matokeo yake mipira ikawa inapigwa kutoka
nyuma kwenda mbele bila mpangilio wa mashambulizi.
Kiwango cha chini walichoonesha Yanga
katika mchezo wa kwanza kimezua wasiwasi kama kwelitimu hiyo itaweza kusonga
mbele ikicheza ugenini. Walizuia vibaya,walipanga mashambulizi vibaya,na hawakuwana
ubora katika mashambulizi.
Saturday, 11 March 2017
MATOKEO: England - Premier League
MATOKEO: Atletico yashinda, Barcelona ugenini, Real nyumbani Leo
March 8
FT Espanyol 4 - 3 Las
Palmas
March 11
FT Valencia 1 - 1 Sporting
Gijon
FT Sevilla 1 - 1 Leganes
FT Malaga 1 - 2 Alaves
FT Granada 0 - 1 Atletico
Madrid
March 12
13:00 Real Sociedad ? - ? Athletic
Bilbao
17:15 Deportivo La Coruna ? - ? Barcelona
19:30 Celta Vigo ? - ? Villarreal
21:45 Real Madrid ? - ? Real
Betis
Subscribe to:
Posts (Atom)