TANGAZA NASI HAPA

Tuesday, 28 February 2017

Tegete na wachezaji wengine walivyotetea kiwango cha Juma Abdul hivi sasa





Na  Baraka  Mbolembole

WACHEZAJI  wa zamani  na  sasa  wameungana  kutetea  kiwango  cha baadhi  ya  wachezaji  wa  Yanga  SC  dhidi  ya  mahasimu  wao  Simba  SC  siku  ya  Jumamosi  iliyopita. Upande  wangu  sikuvutiwa  na  kiwango  cha  mlinzi  wa  kulia  wa  Yanga, Juma  Abdul  kwa  kuzingatia  uwezo  wake  wa  msimu  uliopita  na jinsi  anavyocheza  sasa.

 Mimi  nina  imani na  Juma Abdul  kwasababu  ameshapevuka kimpira, changamoto  na  mambo  ya  soka anayajua  vizuri hivyo  suala la  kurudisha  uwezo wake  wa  awali lipo ndani  ya  uwezo  wake, tumpe muda na  siyo  kumuhukumu.”  Anasema  nahodha  wa  Polisi  Moro  FC, Nahoda  Bakari.

“ Kisa  mechi ya  Jumamosi ndiyo  Juma  alaumiwe? Siku  zote  mlikuwa  wapi ‘kuwajaji’ . kubalini kufungwa hiyo  ndiyo  mechi  ya ‘derby’ hata  Kessy  angecheza kwa  mfano na timu  ingefungwa  wangesema  kwa  sababu  katoka  Simba. Tutajaribu kuangalia  mbali sio  hapa. Tabu  yetu Watanzania ni  kulaumu  tu  ndiyo maana  soka  letu  haliendelei milele.” Anasema mshambulizi  wa  zamani  wa  Yanga, Jerson  Tegete  ambaye  sasa  anaichezea  Mwadui  FC ya  Shinyanga.
“ Mchezaji  huwezi  kudumu moja  kwa  moja katika  kiwango, hata  ulaya  tunaona  wakati  mwingine  wachezaji  wanashindwa itakuwa  hapa  Bongo ambako mnaweza  kukaa miezi  mitatu bila  kulipwa mshahara. Huyo  Juma  kiwango  kimeshuka  lini  au  juzi baada  ya  kufungwa na  Simba?” anahoji  Tegete  mmoja  kati  ya  wafungaji  bora  watatu  wa  muda  wote  katika  ‘Dar-Pacha’

“ Mchezaji ana changamoto kam umecheza ama unacheza mpira utaelewa. Kwa  hapa  Bongo mchezaji anapofanikiwa kulinda  kiwango  chake  walau  kwa miaka  mitano  anastahili pongeza hasa  kwa  kizazi  cha  sasa. “

Mchezaji  anasafiri  kucheza  mechi Bukoba  mpaka  Songea, Mtwara  mpaka  Mwanza na  mshabiki  anataka  kiwango kilekile wakati  viwanja  ni  vibovu, malipo ‘kiduchu’ huku nyumbani familia  ina  matatizo. Kila mechi ina falsafa iliyommeza,tujifunze Mpira.” Anasema kipa  wa  zamani  wa  timu  za Taifa  za  Tanzania  na  klabu  ya Polisi  Morogoro,Madopi  Mwingira  amuunga  mkono Tegete.

“ Ni  kweli  kaka  Madopi, sema  hawajui,ndiyo  maana wanaona  watu wakiwa Simba, Yanga,Manchester  United, Real Madrid hawajui  kuwa  muda  mwingine kuna  mambo  yanakuwa  yakiendelea ndani  ya  klabu. Hatukatai mechi  za  Simba  na  Yanga  kuwa  zinaleta  mawazo sana kutokana  na  ushabiki, lakini tubakize  maneno ya  akiba siyo  kisa  timu  yako  imefungwa basi  utoe  yote.” Anasisitiza  Tegete  ambaye  ameshafunga  magoli  matano  katika  mipambano  ya  Yanga  na  Simba.

“ Mimi  nimecheza  muda  mrefu ligi  ya  Bongo pamoja  na  timu  ya  Taifa, na  sasa  nimeusoma mpira, tujadili  kama  ‘wajuzi’. Simba na  Yanga  ni  kipimo  kizuri kwa  mchezaji  na  timu. Ili mpira uendelee ikiwemo  viwango  vya  wachezaji, haya ndiyo  mambo  muhimu. Moja, ufundi, Pili, waamuzi bora, Tatu, uongozi mathubuti, Nne, wadau, na  Tano  matibabu mazuri. Mimi  nadhani  namba  moja  ndiyo  tuangalie, pia  makocha, tujifunze  soka.” Anasema  Madopi na  kuongeza.
 “ Kwa  mfano, nimzungumzie  Vicent  Andrew ‘Dante’, goli  lililofungwa  na  Laudit  Mavugo, mjuzi  anajua  na  ameona  beki anaangalia kushoto , mshambuliaji yupo nyuma anafnga. Kwangu Danteni miongoni  mwa mabeki bora  wanaochipukia, kiufundi  mchezaji  anatakiwa aangalie  mpira, sehemu  iliyowazi  na  mpinzani  wake. Hapa ndiyo  ufundi  sasa  unahitajika, kuna  principle of  attacks and  defence. Mpira ni  kuzuia na  kushambulia.”
  
“ Madopi  Mwingira, Jerson  Tegete mmetumia vipaji  vyenu juu  ya  soka kumfahamisha kidogo mchambuzi Baraka Mbolembole,nashukuru amewaelewa. Uchambuzi  wa  mpira wa  miguu unahitaji uelewa wa  mpira, uwe  mchezaji, uwe  kocha, daktari, meneja, na  waandishi wa  habari  za  michezo. Umefika  wakati  tuendane  na  wakatisiyo  ‘blablaa’ hiyo  ni  kazi  ya  muda  mfupi zaidi  duniani, imejaa  mizengwe, fitna  na  majungu.” Anasema  mchezaji  nyota  wa  zamani  wa  Taifa  Stars, Athumani  Jumapili  Chama.

“uchambuzi wa mpira wa miguu unaitaji uelewa wa mpira,uwe mchezaji,coach,dk team,meneja team na wahadishi wa michezo hao wana ueledi,uelewa wa football,imefika wakati tuendane na wakati,sio blablaa ndo kazi ya muda mfupi zaidi duniani,imejaa mizengwe,fitna,majungu

‘Tunadaiwa, tutamlipa Vicent Bossou’-Mkwassa




 Na Baraka  Mbolembole

KATIBU  Mkuu  wa  klabu  ya Yanga  SC,Charles  Boniface  Mkwassa  amekiri  klabu  yake kudaiwa  na mlinzi  wa  kimataifa wa  Togo, Vicent Bossou.

Mlinzi  huyo  wa  kati  ilidaiwa  ni mgonjwa  wa nyonga  ndiyo maana  hakupangwa katika  mchezo  wa  kichapo  cha 2-1  kutoka  kwa  Simba SC siku  ya  Jumamosi  iliyopita, lakini  ukweli   mchezaji  huyo  wa  timu  ya Taifa  ya  Togo  aligomea  mchezo  huo  kwa madai  ya  kudai  mishahara  yake  ya  miezi  minne.

“ Nachofahamu  mimi  ni  kwamba  kuna mishahara  ya  mwezi  wa  nane ambayo  ilicheleweshwa, si  kwa  Bossou  tu  ni  timu nzima. Mshahara  wa  mwezi  wa  12  zikiwa  zimebaki  siku  kumi kila  mchezaji  aliandikiwa  cheki, wakalipwa  pamoja  na mshahara  wa  mwezi  wa  kwanza.” Anasema  Mkwassa 

 Kupitia  kurasa  ya  mtandao wake  wa  kijamii  Bossou  aliweka  wazi  kuwa hajalipwa  mshahara  wa miezi  minne  sasa  na  kuutaka  uongozi wake  kumlipa  haraka.

 Sasa  wakati  cheki  zinatoka, Bossou alikuwa alikuwa  kwenye  mashindano AFCON kule  Gabon na  yule  mtoa  cheki hakumkabidhi  mtu  yeyote  cheki  ya  mtu  mwingine  hadi  muhusika  mwenyewe awepo kwa  hiyo cheki  ya  Bossou  ilirudi  ofisini. “

 “ Alivyorejea tulimwambia  afuatilie  cheki  yake lakini  hakwenda na  tumejaribu  kufuatilia  tumeona  kuna  matatizo kidogo. Mshahara  wa  mwezi  wa  pili  kila  mchezaji  bado  hajapokea kama  unavyojua  timu  yetu ina  matatizo  kidogo kwa  mwenyekiti  hivyo mambo mengi  yamesimama.”


VPL: Yanga SC kuivaa Ruvu Shooting Leo bila Donald Ngoma




 Na  Baraka Mbolembole

BAADA  ya  kupokea  kipigo  cha  2-1  kutoka kwa mahasimu  wao  Simba  SC  siku  ya  Jumamosi  iliyopita,mabingwa  watetezi  wa  ligi  kuu  Tanzania  Bara, timu  ya  Yanga  SC  Leo Jumatano  itashuka  uwanja  wa  Taifa  Dar  es  Salaam kuwavaa  Maafande  wa  Ruvu  Shooting katika  muendelezo wa  michezo  ya  ligi  kuu.

 Yanga  ilikuwa  ikijifua  tangu  Jumatatu  lakini  kwa  mara nyingine  wataingiza  timu  yao  uwanjani  bila  huduma  ya  mshambulizi  Mzimbabwe, Donald  Ngoma  ambaye  bado  anasumbuliwa  na matatizo ya  goti.

Ikiwa  na  pointi 49  baada  ya  kucheza  michezo 22 kikosi  hicho  cha  kocha  Mzambia, George  Lwandamina  kitalazimika  kushinda ili  kupunguza  ‘gepu’  la  pointi  tano dhidi  ya  vinara  Simba  ambao  tayari  wamecheza  michezo 23.

Yanga  imeingia  katika  kipindi  kingine  kigumu  msimu  huu  baada ya kupoteza  mchezo  wa  tatu  Jumamosi  iliyopita. Mara  baada  ya  kucheza  na  Shooting  timu  hiyo itasafiri  hadi  mkoani Morogoro  kuwavaa  Mtyibwa  Sugar  katika  uwanja  wa  Jamhuri sehemu  ambayo  wamefanikiwa  kushinda  mara  moja  tu  katika  miaka  nane  iliyopita.

 “  Timu imejiandaa vizuri, naweza kusema  maandalizi  kuelekea  mchezo  wa  Jumatano  hii yameshakamilika. Timu  ilikuwa  ikifanya  mazoezi  tangu  siku  ya  Jumatatu, jana  pia walifanya  mazoezi  ya  jioni sasa  wako  kambini tunasubiri  jioni  waingie  uwanjani kucheza  mechi.”  Anasema  Mkwassa mchezaji  na  kocha  wa  zamani  wa  klabu  hiyo.

“ Sisi  kama  uongozi  tunajua  tunakwenda  kucheza  mechi  nyingine ngumu, vijana  itabidi  wajipange  vizuri ili  kuweza  kupata  matokeo mazuri. Kama  unavyojua  mechi  iliyopita  hatukupata  matokeo  mazuri kwa  hiyo  ili  kuwaamsha  tena  mashabiki  wetu tunahitaji  kupata  matokeo mazuri ili  kurudisha  moto  tuliokuwa nao. Jukumu  kubwa  ni  la  wachezaji pamoja  na  benchi  la  ufundi kuweza  kuamsha  hiyo  morali  na  sisi  kama  uongozi  tuko  nyuma  yao.”

 “ Kuhusu  Donald  Ngoma  ni  kwamba  taarifa  nilizokuwa nazo  ni  kwamba bado  anasumbuliwa  na  majeraha hivyo  hatoweza  kutumika  katika  mchezo  wa  Leo.”

LA LIGA; Valencia yashinda, Betis yaipiga Malaga, Barcelona, Real Madrid uwanjani Leo




REAL Sociedad ililazimishwa  sare  ya  kufungana 2-2 nyumbani Estadio  Anoeta  dhidi  ya Eibar . Juanmi  aliwafungia  wenyeji  goli  la  kuongoza  dakika  ya  14’. Goli  hilo  lilidumu  kwa dakika  12  tu  baada  ya  Gonzalo Escalante  kuisawazishia  Eibar  dakika  ya 26’.

Mchezo  huo ulikwenda  mapumzik  timu  hizo  zikiwa  sare  ya  kufungana  1-1 na  mara  baada  ya  kuanza  kwa  kipindi  cha  pili,  kadi  mbili  nyekundu  zilitolewa. 

Dakika  ya Florian Lejeune alioneshwa  kadi  ya  pili  ya  manjano  na  kuondolewa  uwanjani  upande  wa  Eibar, dakika  ya  59’, Juanmi  wa  Real  Sociedad  naye  akaondolewa  uwanjani  kwa  kati  ya  pili  ya  njano  iliyoambatana  na  ile  nyekundu.

Mshambulizi wa  Mexico, Carlos  Vela  aliwafungia  Sociedad goli  la  pili  kwa  mkwaju wa  penalty na  huku  ikionekana  kama  wageni  wamelala, dakika  ya  tatu  ya  muda  wa  nyongeza Pedro  Leon akaisawazishia  Eibar.
 Katika  mchezo  mwingine  katika  dimba  la  Mestalla, wenyeji  Valencia  walishida  1-0 dhidi  ya Leganes. Goli  pekee  katika  mchezo  huo  lilifungwa na  mlinzi Eliaquim Mangala dakika  ya  29’. Leganes  ilicheza  pungufu  mchezaji  mmoja  kufuatia  kadi  mbili  za  njano  alizooneshwa Alberto. 
 Ikicheza  ugenini  Estadio La Rosaleda, timu  ya  Real  Betis  ilitoka  nyuma 1-0  na  kuishinda  Malaga  katika  mchezo mwingine  uliopigwa  usiku  wa  Jumanne. Pablo Fornals aliifungia  Malaga  goli  la  uongozi  dakika ya 39’.

Jonas Martin aliisawazishia  Betis  dakika  ya  48’ na  zikiwa  zimesalia  dakika  16 mchezo  kumalizika Antonio Sanabria  akafunga  goli  la  ushindi  na  kuwapa  Betis  ushindi 2-1.

MECHI  ZA  LEO KATIKA  LA  LIGA

FT Real Sociedad 2 - 2  Eibar

FT Malaga 1 - 2  Real Betis

FT Valencia 1 - 0  Leganes

March 1

20:30 Barcelona ? - ?  Sporting Gijon

20:30 Osasuna ? - ?  Villarreal

22:30 Celta Vigo ? - ?  Espanyol

22:30 Granada ? - ?  Alaves

22:30 Real Madrid ? - ?  Las Palmas