TANGAZA NASI HAPA

Wednesday, 1 March 2017

LA LIGA: Barca yafanya 'mauaji' yapaa kileleni, Bale alambwa redcard Real Madrid 3-3 Las Palmas



 BARCELONA imepaa  kileleni mwa  msimamo wa ligi kuu  Hispania-La Liga baada  ya  ushindi  wa  magoli 6-1 dhidi  ya  Sporting  Gijon  katika uwanja  wa  Camp Nou; wapinzani wao Real Madrid  ‘wakikwama’ baada  ya  sare  ya 3-3 dhidi  ya  Las  Palmas usiku wa Jumatano hii katika dimba la  Santiago  Bernabeu.
 Leonel Messi 9’, Luis  Suarez 27’ na  Neymar 65’ kila  mmoja  alifunga, goli  la  kujifunga  la  Juan Rodriguez 17’, Paco Alcacer 49’ na  Ivan  Rakitic 87’ walifunga  magolimengine  ya  Barca na  kuwahakikishia  ushindi  mabingwa  hao  watetezi. 

Mwanasoka  bora  wa  dunia  Cristiano  Ronaldo  alifunga  magoli  mawili  ndani  ya  dakika  tatu  za  mwisho  na  kuinusuru  Madrid  kukutana  na  kipigo  mbele  ya Las  Palmas katika  mchezo  ambao  ulishuhudia  staa  wa  Wales, Gareth  Bale  akilambwa  kadi  ya  pili  ya  njano  kisshanyekundu dakika ya 47’.
 Isco  alifunga  goli  la  kuongoza  upande  wa  wenyeji dakika  ya 8’, lakini goli  hilo  lilidumu  kwa  dakika  mbili  tu  kabla  ya Pedro Tanausu Dominguez kuisawazishia  La  Palmas dakika  ya  kumi  na  hadi  kipindi  cha  kwanza  kinamalizika  timu  hizo zilikuwa  sare  ya  kufungana 1-1. 

Jonathan Viera alifunga  goli  la  pili  kwa  njia  ya  mkwaju  wa  penalty  dakika  ya  46’  kufuatia  madhambi  yaliyofanywa  na  nahodha  wa  Real, Sergio  Ramos. Kevin Prince-Boateng akaongeza  linguine  dakika  ya 59’ na  kuwafanya  wageni  kuongoza  3-1.
 C.Ronaldo akafunga  kwa  mkwaju wa penalty  dakika  ya 86’ akaongeza  la  tatu  dakika 89’ na  kuipa sare  ya  3-3  timu  yake. Kwa  matokeo hayo Barcolana  imekwea  kileleni  ikiwa  na  alama  57-pointi moja  mbele  ya  REAL Madrid  ambao  wana  mchezo  mmoja  wa  kiporo.

HAYA  HAPAMATOKEO YOTE  YA  LA LIGA  USIKU  WA  JUMATANO

FT Barcelona 6 - 1  Sporting Gijon

FT Osasuna 1 - 4  Villarreal

FT Celta Vigo 2 - 2  Espanyol

FT Granada 2 - 1  Alaves

FT Real Madrid 3 - 3  Las Palmas

No comments:

Post a Comment